KOSA LANGU

Joyce ni msichana aliyezaliwa katika familia ya watoto wawili akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya Mzee Ndesanjo, maisha yao yalikuwa ni maisha ya furaha na amani walikuwa wakiishi Mkoa wa Dar es salaam maeneo ya Kimara Stop Over, lakini furaha hiyo ilipotea baada ya siku moja ambapo Mzee Ndesanjo alikuja nyumbani baada ya kutoka kazini na moja kwa moja akimtaka mama Joyce ajiandae kwani wangesafiri siku hiyo ambapo ilikuwa ni siku ya jumanne mida ya saa kumi na mbili jioni.Mzee Ndesanjo alikuwa na gari aina Eskudo alifika na kuita kwa sauti "Mama Joyce Mama Joyce" huko chumbani mama Joyce alimskia na kuitika "Bee Mume wangu,vipi mbona unaonge kwa sauti sana si ungeingia ndani kwanza" alisema mamaJocye huku akiwa anamuangalia mume wake kwa makini Baba Joyce alimsogelea huku akisema "hakuna muda wa kupoteza mimi ndani siingii nenda kajiandae tunasafari ya kwenda Morogoro kuna matatizo kwani rafiki yangu tunayefanya naye kazi  amefiwa na mke wake wake inabidi tuwahi kwenda"


mama Joyce alinyamaza kimya kidogo kana kwamba kuna kitu anatafakari na kusema "mmmh jamani ni nini tena kilimfika kwani alikuwa anaumwa masikini" aliongea kwa masikitiko Baba Joyce akamjibu na kusema "alikuwa anaumwa na ameugua kwa muda mfupi sana,wewe nenda kajiandae tuondoke"  mama Joyce akasema "Lakini mume wangu watoto tutawaacha na nani" aliuliza mama Joyce kwani kwa wakati huo Jocye na mdogo wake aliyeitwa James walikuwa wameenda shule Joyce alikuwa darasa la tano na James akiwa darasa la kwanza na pale walipokuwa wakiishi likuwa ni nyumba ya kupanga.Baba Joyce alimgeukia tena mke wake na kusema "hawa watoto tutamkabidhi jirani yetu Mzee Ngonyani na mkewe kwani hatuendi kukaa zaidi ya siku mbili wewe jiandae tuondoke wakirudi kutoka shule watakuta maagizo kutoka kwa mke wa Ngonyani" alisema baba Joyce.

Ndipo mama Joyce akaenda kwenye chumba cha Mke wa Ngonyani na kumwachia maagizo ya kuwaangalia watoto wake kwa kipindi cha siku mbili baada ya hapo aliingia chumbani na kujiandaa tayari kwa safari ambapo safari ilianza wakiwa njiani maeneo ya  Kidatu ghafla gari lilipata pancha tairi ya mbele na kupinduka ilikuwa ni ajali mbaya sana kwani Baba Joyce alifariki palepale na Mama Jocye alikuwa ameumia sana sehemu za kichwani hivyo wasamaria wema walimchukua na kumkimbisa hospitali,,,,nini kilitokea itaendelea